Kiswahili Quiz 1

0%
23

KISWAHILI QUIZ 1

Chozi la Heri

Jibu maswali kulingana na maagizo yaliyopewa

Andika jina lako na barua pepe katika nafasi ulioachiwa hapo.

1 / 15

Tambua msemaji wa maneno haya: 'Vijulanga vilinyakuliwa kwa lazima kutoka kwenye susu zao, hata vifua havijapanuka...'

2 / 15

Tambua mbinu zozote mbili zinazojitokeza katika dondoo hili: 'Uvuguvugu uliotokana na mwanguko wa machozi haya uliulainisha moyo wake ukampa amani kali.'

3 / 15

Tambua msemaji wa maneno haya: 'Ni muhimu pia ujue kwamba ikiwa unataka kujiokoa au kuzoea hali mbaya inayokukabili, ni muhimu kujiingiza katika hali yenyewe,'

4 / 15

Taja msemaji wa maneno haya: 'Unajua hali ya mtafaruku wa kihisia inayowapata vijana katika umri huu.'

5 / 15

Tambua msemewa wa maneno haya: ' Hawezi kumdhuru. Simba hata akawa mkali vipi ni muhali kumrarua mwanawe'

6 / 15

Taja msemaji wa maneno haya: 'Unajua hali ya mtafaruku wa kihisia inayowapata vijana katika umri huu.'

7 / 15

Tambua mbinu inayojitokeza katika dondoo hili: 'Baada ya kiviga hiki, mimi,mama na ndugu zangu wengine tuliendelea na safari bila kujua kipaji na kisogo cha safari yenyewe'

8 / 15

Tambua msemaji wa maneno haya: Si nyinyi mliokuwa hata mkipinga elimu ya mabinti hawa?'

9 / 15

Tambua mbinu zozote mbili zinazojitokeza katika dondoo hili: 'Vipi dume kubwa kama wewe litafuata mkondo kama maji bila nadhari?'

10 / 15

Tambua mbinu zozote mbili zinazojitokeza katika dondoo hili: 'Hata hivyo walikuwa wapiga mbizi nchi kavu, maskini wakaishia kuumiza nyuso zao! Maandamano yao yalisalimiana na risasi na vitoza machozi.'

11 / 15

Tambua msemaji wa maneno haya: "Hakuna amani bila kumheshimu mwanaume"

12 / 15

Taja mrejelewa wa maneno haya: 'Mambo ya sudi huenda kwa sudi'

13 / 15

Tambua msemewa wa maneno haya: 'Huku kutakuwa kukata mbeleko kabla ya mtoto kuzaliwa'

14 / 15

Tambua msemaji wa maneno haya: '...msafiri wa kikaida huwa kafiri, sembuse sisi ambao tulisafiri bila hiari!'

15 / 15

Tambua mbinu ya uandishi inayojitokeza katika dondoo hili: "Alijiona kama mfa maji ambaye anakabiliwa na mtutumo wa mawimbi ya misiba, mmoja baada ya mwingine."

Your score is

The average score is 25%

0%